Diagnostics

AdBlue Ni Nini?

AdBlue ni kiowevu maalum (diesel exhaust fluid) kinachotumika kwenye baadhi ya magari ya dizeli ya kisasa kupunguza uchafuzi wa hewa (nitrogen oxides) kupitia mfumo unaoitwa SCR (Selective Catalytic Reduction). AdBlue hutumika kidogo kidogo wakati gari linatembea na huhitaji kuongezwa mara kwa mara.

AdBlue warning inapowaka, mara nyingi inamaanisha kiwango cha AdBlue kimepungua na kinahitaji kuongezwa. Katika baadhi ya matukio, tatizo laweza kuwa la sensa au mfumo wa SCR wenyewe badala ya kiwango cha kiowevu.

Kupuuzia AdBlue warning kwa muda mrefu kunaweza kusababisha gari kushindwa kuwaka kabisa kwa sababu za kisheria za uchafuzi wa hewa. Kama huna uhakika chanzo cha warning, uchunguzi wa Auto Diagnostics unaweza kubaini kama ni suala la kiowevu au la mfumo wa SCR.

Huduma Zinazohusiana

Unahitaji huduma hii?

Soma Pia

Makala Nyingine

📱 📞
Tuachie namba yako

Tutakupigia au kukutumia ujumbe kuhusu huduma unayohitaji — haraka na bila malipo.

Asante! Tutawasiliana nawe hivi karibuni.