Uchunguzi na ushauri wa matengenezo ya injini.
Uchunguzi na ushauri wa matengenezo ya injini.
Kama gari lako "linagoma kuwaka" au injini haifanyi kazi vizuri, sisi ni fundi wa engine Mwanza tunaofanya uchunguzi wa kina kabla ya kupendekeza ukarabati.
Kabla ya kufanya ukarabati wowote, tunapima gari kwa computer kubaini fault codes halisi zinazotoka kwenye ECU. Hii inatusaidia kukupa jibu sahihi badala ya kukisia, na kuepusha gharama za kubadilisha vipuri visivyohusika na tatizo.
Huduma hii inatolewa Mabatini, Mwanza. Kwa maelezo zaidi au kuweka miadi, wasiliana nasi kwa simu, WhatsApp au fomu iliyo hapa chini.
Fault codes zinaonyesha chanzo halisi cha tatizo — hii inapunguza gharama na muda wa kutafuta tatizo kwa majaribio.
Kwa magari mengi, uchunguzi wa awali unakamilika ndani ya dakika chache; muda unaweza kuongezeka kama tatizo linahitaji uchunguzi wa kina zaidi.
Tutakupigia au kukutumia ujumbe kuhusu huduma unayohitaji — haraka na bila malipo.
Asante! Tutawasiliana nawe hivi karibuni.